WATU
mbalimbali leo walikusanyika nyumbani kwa marehemu Amina Athuman Ukonga
Banana, Dar es Salaam kutoa heshima za mwisho kabla ya mwili wake kusafirishwa
kwenda kuzikwa Tanga kesho.
Akizungumza
kwa niaba ya wandishi wa habari za michezo, Mwenyekiti wa Chama cha Wandishi wa
habari, Juma Pinto alisema tasnia imeondokewa na mwandishi mchapakazi na
mwadilifu.
“Kwa niaba
ya wandishi wa habari za michezo tumepokea kwa masikitiko msiba wa Amina kwani
alikuwa mchapakazi na alipenda kushirikiana na wenzake,” alisema Pinto.
Naye Kaimu
Mkurugenzi wa Kampuni ya Uhuru Publications, Angela Akilimali alisema
wamepoteza mfanyakazi hodari na pengo lake halitazibika.
“Amina
alipatwa na umauti wakati akitimiza wajibu wake visiwani Zanzibar hiyo
inadhihirisha wazi alikuwa mfanyakazi anayependa kutimiza wajibu wake bila
kujali hali yake,” alisema Angela.
Amina
alikuwa visiwani Zanzibar kikazi, kuripoti michuano ya Kombe la Mapinduzi na
Mwenyezi Mungu akamuongoza kuifanya kazi yake vizuri mwanzo hadi mwisho.
Amina
alipatwa na umauti usiku wa kuamkia Jumapili akiwa amelazwa khospita na alijifungua mtoto wa
kiume ambaye kwa bahati mbaya alikwishafariki dunia.
Amina
ameacha motto mmoja wa kike. Mungu ampumzishe kwa amani Amina Athumani.
No comments:
Post a Comment