ALIYEKUWA
Kocha wa timu ya Taifa, ‘Taifa Stars’ Charles Mkwassa amesema kilio chake
kimesikika na hatimaye Tanzania imepangwa kwenye kundi rahisi kuwania kufuzu
Kombe la mataifa Afrika mwaka 2019.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mkwassa ambaye ameifundisha Taifa Stars akiridhi mikoba ya kocha Mdenmark Mart Nooij amesema timu ambazo zipo kundi moja na Tanzania ni rahisi ukilinganisha na kundi la msimu uliopita ambapo ilipanga na Nigeria na Misri.

“Timu
zilizopangwa kundi moja na Tanzania ni timu za kawaida ukilinganisha na Misri
au Nigeria lakini maandalizi ya mapema ni muhimu ili kufanya vizuri,” alisema
Mkwassa
Pia Mkwassa alisema pamoja na kuonekana kuwa
rahisi lakini kitendo cha nchi hizi kuwa na viwango vinavyokaribiana kinaweza
kufanya iwe ngumu zaidi kwa maana ya kukamiana.“jukumu linabaki kwa shirikisho la Soka (TFF), wachezaji pamoja na benchi la kiufundi kujiandaa kwani nilisema hadharani tumekuwa tukipangwa kwenye kundi la kifo ila droo ya sasa CAF walisikia kilio changu na inawezekana iwapo tutaamua,” alisema Mkwassa.
Tanzania
imepangwa kundi moja na vinara wa soka ukanda wa Afrika Mashariki Uganda, Lesotho
na Cape Verde, kundi L ambalo wadau wengi wanasema ni ahueni endapo maandalizi
yataanza mapema.
Kwa upande
wa timu ya Taifa ya Kenya 'Harambee Stars' ambayo ipo ukanda huu wa Afrika
Mashariki imepangwa kundi F sambamba na Ghana, Ethiopia na Sierra Leone.
Wenyeji wa michuano hiyo Cameroon ambayo imefuzu moja kwa moja imepangwa kundi B pamoja na Morocco, Malawi na mshindi kati ya Comoro na Mauritius.
Wakati huo huo timu za Sao Tomé, Madagascar, Comoro, Mauritius, Djibouti na Sudan Kusini wataanzia kwenye mechi za mtoano Machi na mataifa matatu yataingia kwenye hatua za makundi.

Jinsi makundi
yalivyopangwa:
Kundi A: Senegal, Equatorial Guinea, Sudan, Sao Tome/Madagascar
Kundi B: Cameroon, Morocco, Malawi, Comoro/Mauritius
Kundi C: Mali, Gabon, Burundi, Djibouti/Sudan Kusini.
Kundi D: Algeria, Togo, Benin Gambia.
Kundi E: Nigeria, Afrika Kusini, Libya, Shelisheli.
Kundi F: Ghana, Ethiopia, Sierra Leone, Kenya.
Kundi G: DR Congo, Congo Brazzaville, Zimbabwe, Liberia.
Kundi H: Ivory Coast, Guinea, Jamhuri ya Afrika ya kati, Rwanda
Kundi I: Burkina Faso, Angola, Botswana, Mauritania.
Kundi J: Tunisia, Misri, Niger, Swaziland.
Kundi K: Zambia, Msumbiji, Guinea-Bissau, Namibia.
Kundi L: Cape Verde, Uganda, Tanzania, Lesotho.

No comments:
Post a Comment