NDEJEMBI AMBANA MKANDARASI ANAYEJENGA NJIA YA 220 KILOVOTI KUTOKA SONGEA HADI MASASI



Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, amemwonya mkandarasi anayetekeleza mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 220 kutoka Songea hadi Masasi kupitia Tunduru, kuhakikisha anaongeza kasi ya utekelezaji wa mradi huo ili ukamilike kwa wakati uliopangwa.

Onyo hilo amelitoa wakati wa ziara yake ya kikazi katika Wilaya ya Tunduru, ambapo alikagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo na kupokea taarifa kuhusu hatua zilizofikiwa pamoja na changamoto zinazojitokeza.

Mhe. Ndejembi alisema Serikali haitavumilia ucheleweshaji wa miradi ya kimkakati, akisisitiza kuwa mradi huo una umuhimu mkubwa katika kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika, kuchochea shughuli za uzalishaji, kuvutia uwekezaji na kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa mikoa ya Ruvuma na Mtwara.

No comments