KLABU ya
Manchester United leo imefanyia kweli katika raundi ya tatu ya Kombe la FA
baada ya kuifunga Reeding kwa mabao 4-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja
wa Old Trafford.
Wakati Man
United ikifanya mauaji hayo katika mchezo huo, vinara wa Ligi Kuu ya England,
Chelsea wenyewe watashuka dimbani kesho kucheza dhidi ya timu ya daraja la tatu
ya Peterborough United.
Mabao ya
washindi katika mchezo huo wa yamefungwa na nahodha wa Man United Rooney
katika dakika ya saba, Martial katika dakika ya 15 huku Rashford akitupia
mawili katika dakika ya 75 na 79.
No comments:
Post a Comment