SERIKALI ya Tanzania na Afrika Kusini
zimekubaliana kushirikiana katika nyanja ya filamu, haki za ubunifu pamoja na
kuandika historia ya ukombozi kusini mwa bara la Afrika.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alisema yeye pamoja na Waziri
wa Utamaduni wa Afrika Kusini, Nathi Mthethwa wamekubaliana kushirikiana kwenye
eneo la sanaa.
“Afrika Kusini
wameendelea kwa upande wa sanaa ndio maana unaona wasanii wengi hapa nchini
wanakwenda kutengeneza filamu huko hivyo tumekubaliana kushirikiana kwani
sheria wamefanikiwa kutengeneza mifumo ya kisheria ya kulinda haki za wasanii
na ubunifu,” alisema Nape.
Pia Nape alisema Serikali ya Tanzania pamoja na
Afrika Kusini mwaka 2011 waliingia
makubaliano ya kushirikiana, jambo ambalo lilifuta viza na kukubaliana kuandaa
historia ya kupigania uhuru kwa nchi za kusini mwa bara la Afrika.
Nape alisema makubaliano hayo yataleta mabadiliko
katika sanaa kwa nchi yetu na kuongeza mahusiano ya nchi mbili kwa watu kwa
watu na siyo nchi kwa nchi.
Moja ya makubaliano hayo ni kutengenezwa route of
indepence kwa sababu isipoandikwa na nchi husika wengine wanaweza wasiiandike
vizuri au wakaikosea na kwa mwaka huu wa fedha imetengewa Sh mil 700.
Waziri Nathi yupo nchini na ujumbe wa watu saba na
jana wamekwenda Morogoro kutembelea makaburi ya Mazimbu na Dakawa na watakwenda
Bagamoyo pamoja na Dar es Salaam, ambapo watatembelea jengo ambalo lilikuwa
likitumika kwa vikao vya kupigania uhuru lililopo pembeni ya jengo la ubalozi wa Msumbiji.
Mwanzo jengo hilo lilikuwa linatunzwa na jeshi
lakini kwa sasa lipo chini ya Wizara ya Habari na lipo kwenye mpango wa
kukarabatiwa.
No comments:
Post a Comment