FAINALI
ya msimu wa pili wa shindano
la kusaka vipaji vya sanaa ya ucheshi linatarajiwa kufanyika leo katika ukumbi wa
40/40 Tabata, Dar es Salaam.
Jumla ya washiriki 18 waliopatika na kutoka wilaya
za mkoa wa Dar es Salaam watapanda jukwaani kuonesha vipaji vyao na fainali
hizo ni bure.
Akizungumza na gazeti hili
Meneja wa Vuvuzela Company Ltd, Evans Bukuku alisema shindano hili litaendelea, kwani sanaa ya ucheshi inaweza kutengeneza
nafasi kubwa kwa Watanzania wengi.
“Mshindi atapata
pesa taslimu 2,000,000/= na mafunzo ya vitendo ya miezi 6
Mashindano haya yalianza Septemba
6, 2016 yakijumuisha zoezi la kusajili washiriki na fainali hizo zitasindikizwa
na burudani kutoka Twanga Pepeta Band na kiingilio ni bure kwa watu waliotimiza
miaka 18 na kuendelea.
No comments:
Post a Comment