KAMATI ya
Rufaa ya Shirikisho la Soka Tanzania, imefuta uchaguzi wa Chama cha Soka mkoa
wa Iringa (IRFA) na kuagiza mchakato kuanza upya ndani ya siku 14.
Akizungumza
na wandishi wa habari, Mwenyekiti wa kamati ya Rufaa ya Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) Dk. Mutabazi Rogazia, alisema kamati yake ambayo ilikutana
Novemba 13 ilipokea rufaa mbili toka mkoa wa Iringa zikipinga uhalali wa
uchaguzi huo.
“Mchakato wa
uchaguzi ulikuwa batili hivyo utangazwe
upya pamoja na taratibu za uchukuaji fomu ziane upya hata wale ambao
hawakuchukua fomu wanaruhusiwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi na mchakato huu
utaanza Novemba 20”, alisema Dk Rogazia
Pia Dk.
Rogazia aliagiza Shirikisho la soka (TFF) lipeleke wajumbe wengine kusimamia
uchaguzi na zoezi zima la mchakato kwani
uwepo wa Juma Lalika kwenye kamati ya uchaguzi kunabatilisha zoezi zima kwani
kwa vile ni mjumbe wa kamati ya Utendaji ya TFF na pia ni mjumbe wa kamati ya
utendaji ya mkoa huo
Dk. Rogazia
alisema kamati yake ilipokea rufaa ya Festo Mkemwa ikipinga Kamati ya Soka ya
Mkoa wa Iringa, kumpitisha Syprian Kuyava ambaye ni Mwenyekiti aliyekuwa
anamaliza muda wake kugombea tena nafasi ya Mwenyekiti mkoa huo.
Na rufaa
nyingine ilikatwa na Ramadhan Mahano, akipinga kamati ya mkoa kumpitisha
Abdulsufiani Omar kuwa mgombea wa nafasi ya uchaguzi wa TFF.
Dk. Rogazia
alisema wakata rufaa wote walipinga maamuzi ya kamati kumpitisha wagombea hao
kwa sababu hawakuwa na uzoefu wa kuongoza wa miaka mitano pia mwenyekiti
aliyemaliza muda wake hakuwahi kuitisha kikao hata kimoja katika vile viakao
ambavyo vipo kisheria.
Mjibu rufaa
Kuyava alijitetea na kupinga kwani aliwahi kuwa kiongozi wa Hazina sports
club ya Dar es Salaam mwaka 2008 na alichaguliwa tena 2011 hadi sasa lakini hakuwahi kuleta uthibitisho
kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi wa kuwa aliwahi kuongoza timu hiyo hadi mchakato wa uchaguzi unamalizika.
Pia Dk.
Rogazia alisema swala la kuwepo kwa vikao lilitibitishwa na Juma Lalika ambaye
ni mjumbe wa kamati ya Utendaji ya TFF, huku pia akiwa ni mjumbe wa kamati ya
utendaji ya mkoa huo na wakata rufaa wakishindwa kuthibitisha rufani zao.
Uchaguzi huo
umebatilishwa na kamati ya rufaa kwasababu Juma Lalika hakusatahili kuwa mjumbe
wa kamati ya utendaji ya TFF na ya mkoa hapohapo tena anakuwa mjumbe wa kamati ya
Uchaguzi ya TFF.
Endapo
wakati wa zoezi la uchaguzi kutatokea kwa zoezi la upigaji kura na matokeo yake
ama kwa moja kwa moja au kwa taswira yake jambo hilo litachukuliwa kwa uzito
wake na kuagiza kamati zote za uchaguzi za TFF kuepuka kufanya mambo ambayo
yapo kinyume na katiba.
No comments:
Post a Comment