SHIRIKA
lisilo la Kiserikali la Karibu Tanzania Association (KTA) kwa kushirikiana na
Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) linaendesha kozi ya awali ukocha wasichana
na wanawake.
Akizungumza
na wandishi wa habari jana Mkurugenzi wa Maendeleo wa KTA, Mia Mjengwa alisema
kozi hiyo inashirikisha makocha 25 toka kwenye vyuo vya maendeleo ya jamii
mbalimbali vilivyopo hapa nchini.
“Tumeanzisha
program hii ili kuwapa fursa zaidi watoto wa kike na wanawake kujifunza soka
kwenye jamii zao na tutakuwa tunatumia vuo vya maendeleo ya jamii kufundisha”,
alisema Mia.
Pia Mia
alisema kuwa kwa kushirikisha vyuo vya maendeleo ya jamii wanaamini kuwa jamii
inapata fursa ya kufundishwa kwa karibu kwani vyuo hivyo vinafanya kazi karibu
na jamii.
Mia alisema
program hii ndio inaanza kwa kuwafundisha makocha na pia itakuja awamu nyingine
kwa ajili ya kuwafundisha waamuzi.
Kozi hiyo ya
siku 10 inafundishwa na mkufunzi wa CAF, Wilfred Kidao.
No comments:
Post a Comment