WAZIRI wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amesema serikali ya awamu ya tano itahakikisha
mashindano ya ulimbwende yanakuwa na thamani na yenye faida.
Nape aliyasema hayo wakati
akimkabidhi bendera ya Taifa, Miss Ilala 2016, Julitha Kabete ambaye pia ni
mshiriki wa mashindano ya Miss Tanzania 2016, ambaye anakwenda kushiriki
mashindano ya urembo Afrika yatakayofanyika Novemba 26 katika kitongoji cha Calabar
kilichopo Nigeria.
“Tunataka mashindano
ya Miss Tanzania ambaye anafaidika sio mshindi peke yake tumeona hapa huyu
alikuwa mshindi wa nne na amepata nafasi ya kuwakilisha nchi, tunafahamu
mashindano ya Miss Tanzania yalikuwa yamefungiwa kufanyika ila sasa yamerudi
vizuri, tutaendelea kuyaimarisha yawe
bora na matarajio ya serikali ni kuona tunakuwa tunafanya vizuri na siku moja
hata mshindi wa Miss World atoke Tanzania,” alisema Nape.
Pia Nape alisema serikali
inamtakia safari njema na ipo nyuma yake kumpa msaada pindi unapohitajika.
Akizungumza wakati wa kukabidhiwa
Miss Julitha Kabete amesema amejiandaa kwa ajili ya mashindano hayo na anaamini
atafanya vizuri kwenye mashindano hayo ambayo ndio kwanza yaanza
“Naomba Watazania wanisapoti ili nifanikiwe
kushinda Miss Africa ambayo inafanyika Nigeria, ni nafasi ya kipekee ambayo
nimepata na nikipata ushindi ni wetu sote,” alisema Julitha.
Mashindano hayo yatafanyika kwa
mara ya kwanza Afrika nayatafanyika katika kitongoji cha Calabar kilichopo
Nigeria.
No comments:
Post a Comment