Pages

Wednesday, September 21, 2016

KILIMANJARO QUEENS MBABE WA CECAFA, KUWASILI KESHO






TIMU ya Taifa ya wanawake ya Tanzania 'Twiga Stars' imeibuka mabingwa wa michuano inayoshirikisha nchi wanachama wa CECAFA baada ya kuichapa Kenya mabao 2-1 kwenye mchezo wa fainali.

Michuano hiyo ambayo ndiyo imefanyika kwa mara ya kwanza katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati imeshuhudia Twiga wakiweka rekodi kwa kuibuka mabingwa wa kwanza.

Twiga ilipata bao la kwanza kupitia mshambuliaji Mwanahamisi Omari dakika ya 39 baada ya kuichambua safu ya ulinzi ya Kenya kabla ya kufunga bao maridadi.

Dakika tano baadae Mwanahamisi tena aliwanyanyua Watanzania kwenye viti baada ya kufunga bao la pili kwa mpira wa adhabu upande wa kushoto wa uwanja kutokana na mchezaji mmoja wa Kenya kufanya madhambi.

Kipindi cha pili Kenya walikuja juu kwa kulisakama lango la Twiga ambapo dakika ya 48 Christina Nafula aliipatia bao la kufutia machozi kufuatia mabeki ya Twiga kuzembea kuondoa hatari.
Safari ya ubingwa wa Kilimanjaro Queens ulianzia hatua ya makundi kwa kuilaza Rwanda manbao 3-2 kabla ya kutoka sare tasa na Ethiopia ambayo pia ilivuna ushindi wa mabao 3-2 kutoka kwa Rwanda. Tanzania na Ethiopia zilitoka sare na kurusha sarafu ambako Tanzania ikawa ya kwanza katika kundi B hivyo kucheza na Uganda ambayo ililala kwa mabao 4-0 katika mchezo wa nusu fainali. Na leo Septemba 20, 2016 ikatawazwa kuwa mabingwa kwa ushindi wa mabao 2-1.
Timu zote shiriki zilikuwa Tanzania, Burundi, Zanzibar, Kenya, Ethiopia, Rwanda pamoja na mwenyeji Uganda. Mashindano ya Kombe la Chalenji la CECAFA kwa timu za wanawake yamefanyika kwa mara ya kwanza jambo linaloleta tafsiri kuwa michuano hiyo inaweza kuinua soka la wanawake kwa ukanda wa nchi za Afrika Mashariki na Kati.

No comments:

Post a Comment