Pages

Wednesday, September 21, 2016

TOTO AFRICAN NA AFRICAN LYON HAKUNA MBABE



TIMU ya African Lyon imebanwa mbavu baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na Toto African katika mchezo wa muendelezo wa ligi kuu  Tanzania bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Lyon ilianza mchezo kwa kuonesha dhamira ya dhati ya kupata alama zote tatu kutokana na kushambulia kwa kasi lango la Toto lakini umakini mdogo wa safu yao ya ushambuliaji ulikuwa kikwazo.

Dakika ya 22 Toto walikosa goli la wazi baaada ya Reliant Lusajo kumpigia pasi safi Waziri Junior lakini shuti lake lilipaa juu ya lango la Lyon ambapo endapo angetulia basi angeweza kuwainua 'Wanakishamapanda' vitini.

Nahodha wa Lyon Baraka Jaffar alimanusura awapatie wenyeji bao dakika ya 62 baada kupiga kichwa kilichopaa juu kidogo ya lango  kutokana na kufanya shambulio kali golini mwa Toto.

Katika mtanange huo Lyon ilimtoa mshambuliaji Hood Mayanja na kumuingiza Peter Mwalyanzi huku Toto ikimpumzisha Jamal Sudi nafasi  yake ikichukuliwa na Hamadi Mumba.

Licha ya kosa kosa za hapa na pale lakini hadi dakika 90 zinakamilika si wenyeji Lyon wala Toto walioweza kupata bao

No comments:

Post a Comment