Pages
▼
Thursday, September 22, 2016
TANZANIA KUJENGEWA UWANJA WA KISASA WA MCHEZO WA MAGONGO
RAIS wa Shirikisho la mchezo wa Magongo Ulimwenguni (FIH) ) Leondro Negre ameahidi kuijengea Tanzania uwanja wa kisasa wa mchezo huo.
Akizungumza na wandishi wa habari jana, Negre alisema FIH kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania watajenga uwanja wa mchezo huo ili kurudisha hadhi ya mchezo kama ilivyokuwa zamani.
“Sisi Shirikisho la Magongo la dunia kwa kushirikiana na serikali tunaahidi kujenga uwanja wa kisasa, serikali itatoa ardhi na sisi tutagharamia ujenzi na shirikisho la Magongo Afrika litaweka miundo mbinu yote”, alisema Negre.
Naye Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye, alimshukuru Negre na kuahidi wizara yake itawasiliana na wizara ya ardhi kwa ajili ya kupata eneo litakalojengwa uwanja huo.
“Nawashukuru viongozo hawa wa mchezo wa Magongo wa dunia na Afrika kwa kuja kunitembelea ofisini kwangu lakini niwaahidi kuwa wizara itashirikiana nao kuhakikisha wanafanikisha azima yao”, alisema Nape.
Mchezo wa Magongo ni mchezo ambao unachezwa kwa kutumia fimbo maalum na unachezwa na wanaume na wanawake na kwenye mashindano ya Afrika yaliyofanyika Afrika Kusini mwaka jana timu ya Tanzania ya wanawake ilishika nafasi ya nne huku wanaume wakishika mkia.
No comments:
Post a Comment