ZIARA YA MAFUNZO NAIROBI
TASWA
kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Kenya, vimeanzisha
program ya ziara ya mafunzo na kubadilishana uzoefu baina ya vyama hivyo viwili,
ikiwa katika makundi tofauti ya wahariri/waandishi waandamizi na kundi lingine
la waandishi wa habari chipukizi.
Kwa
kuanzia wahariri wa habari za michezo 18 au wale wenye uzoefu katika uandishi
usiopungua miaka kumi kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini wataenda Nairobi
kwa ziara ya mafunzo kuanzia Julai 6-9 mwaka huu.
Tunaamini
wakirudi wataendelea kuwa waalimu wazuri kwa wale chipukizi, ambao nao watapata
fursa kama hiyo siku za usoni.
Post a Comment