SHIRIKISHO
la mpira wa miguu barani Afrika (CAF) limetuma leseni za wachezaji wanne wapya
waliosajiliwa na mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Yanga Wachezaji
waliotumiwa leseni hizo ni Hassani Kessy,Beno Kakaolanya, Andrew Vincent na
Juma Mahadhi ambao sasa wanaweza kuitumikia Yanga katika michuano ya ndani na
nje.
Ofisa Habari wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, Alfred Lucas amethibitisha kupokea leseni hizo toka CAF na kusema kuwa wachezaji hao wanaweza kuitumikia klabu hiyo katika michuano mbali mbali.
"Ni kweli tumepokea leseni za wachezaji hao toka CAF zinazowawezesha kuitumikia klabu hiyo katika michuano ya ndani na nje" alisema Alfred.

Wachezaji
hao walisafiri na kikosi cha Yanga kilichokwenda kuweka kambi nchini Uturuki
kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya Mo Bejaia ya
Algeria.
Yanga inaondoka leo Uturuki kuelekea Algeria tayari kwa mtanange huo utakaopigwa siku ya Jumapili.

No comments:
Post a Comment