SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF) limewataka
mashabiki kuwa wazalendo kwa kushangilia kistaarabu timu ya Taifa ya Vijana
'Serengeti Boys na ule wa Yanga kwani zinawakilisha taifa letu.
Akizungumza
na wandishi wa habari jana, Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, Alfred
Lucas, TFF inawaomba mashabiki waje kwa wingi uwanjani kwa ajili ya kushangilia
kwani wanaamini mashabiki ni mchezaji wa 12 na uwepo wao utaongeza ari ya
ushindi.
"Tunafahamu
mchezo wa Yanga utakuwa na changamoto zake kwa vile wameanza kwa kufungwa na TP Mazembe
wanaongoza kundi lakini tunaamini watafanya vizuri kwani inachezwa kwa mtindo
wa ligi hivyo mashabiki waje kushangilia timu zetu.", alisema Lucas.
Yanga
itacheza na TP Mazembe Juni 28 kwenye mchezo wa Kundi A wa kombe la shirikisho barani
Afrika na Serengeti Boys itacheza na Shelisheli mchezo wa kuwania kufuzu
fainali za vijana barani Afrika, Jumapili
Mchezo wa
Yanga utachezwa na mwamuzi wa kimataifa toka Zambia, Janny Sikazwe na atasaidiwa
na Jerson Emiliano toka Angola na Berhe O'Michael toka Eritrea wakati mezani
atakuwepo Wellington Kaoma toka Zambia.
Kamishna wa mchezo
huo ni Celestin Mtagungira toka Rwanda wakati mratibu wa mchezzo huo ni Sidio Mugadza toka Msumbuji.
Kwa upande
wa Serebgeti Boys, mchezo huo utachezeshwa na waamuzi toka Ethiopia ambao ni
Belay Asserese akisaidiwa na Tigle Bilachew na Kinfe Yilma na mezani atakuwepo
Lemma Nigussie na kamishina atakuwa Kalombo Bester toka Malawi.
Yanga
inatarajia kurejea nchini wakati wowote ikitoka Algeria ambapo ilikwenda
kucheza na Mo Bejaia ambapo ilifungwa bao 1-0.
No comments:
Post a Comment