Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, June 18, 2016

MRITHI WA DUNGA NI TITE ‘ANAAMINIKA’


LEJENDARI wa Brazil Pele amesema kuwa Kocha Mpya wa Timu ya Taifa ya Brazil Tite ni Mtu anaeaminika.
Jumatano CBF, Shirikisho la Soka la Brazil, lilimteua Tite, mwenye Miaka 55, kuchukua nafasi ya Dunga alietimuliwa hivi Majuzi baada ya Brazil kushindwa kusonga kutoka Hatua ya Makundi ya Copa America Centenario walipofungwa 1-0 kwa Bao la utata na Peru huko USA.
Tite, ambae Jina lake kamili ni Adenor Leonardo Bacchi, ataacha kuifundisha Klabu ya huko Mjini Sao Paulo, Brazil, Corinthians, ambayo ametwaa nayo Mataji kadhaa, ili kushika hatamu Timu ya Taifa ya Brazil.

Pele aliongea na Wanahabari Jana Mjini Santos, Brazil kwenye Jumba la Makumbusho ya Pele ambako alikuwa akitunukiwa Tuzo ya Juu, Olympic Order, kutoka Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, IOC, aliyokabidhiwa na Rais wake Thomas Bach.

Brazil ndio Wenyeji wa Michezo ya Olimpiki itakayochezwa Nchini humo Mjini Rio de Janeiro kuanzia Agosti 5 hadi 21.

Pele alisema: “Tite ni mtu anaeaminika.”

A Brazil fan watches the Copa America Centenario match
Kuhusu Dunga, Pele alisema Dunga hakuwa na makossa kwani hakuwa na muda kuitayarisha Timu na kufungwa ndio Soka.
Tite amezifundisha Klabu kubwa kadhaa huko Brazil zikiwemo pia Gremio, Atletico Mineiro na Palmeiras, na pia huko Falme za Nchi za Kiarabu kwenye Klabu za Al Ain na Al Wahda. 

No comments:

Post a Comment