Jeremia Juma akituliza mpira wakati wa mazoezi ya timu ya Taifa 'Taifa Stars' hivi karibuni |
MSHAMBULIAJI wa Tanzania Prisons, Jeremia Juma amekiri kuwa kwenye mazungumzo na Simba lakini hatakuwa tayari kupoteza ajira yake kwa kiasi kidogo cha pesa.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, mshambuliaji huyo ambaye msimu uliopita alifunga mabao 14 katika ligi kuu Tanzania Bara amesema yeye ni mwajiriwa wa jeshi la magereza hivyo anahitaji pesa ambayo itamshawishi kumvua magwanda yake.
“Ni mapema mno kusema kama nitaachana na kazi yangu ya sasa, muda ukifika nitawaambia kwani nipo tayari kuichezea timu yoyote ambayo itanipa hela ninayohitaji siyo Simba pekee bali nipo kwenye mazungumzo na klabu nyingine”, alisema Jeremia.
Pia Jeremia alisema klabu nyingine wameshindwana kwenye maslahi na kuachana nao lakini mazungumzo na Simba yanaendelea kupitia mtu wake wa karibu.
Jeremia ameonekana
kufanya vizuri katika soka akiridhi kipaji alichokuwa nacho baba yake Juma
Mgunda ambaye alikuwa hodari katika kufunga mabao wakati akichezea Coastal
Union ya Tanga na timu ya Taifa.
No comments:
Post a Comment