Siku moja baada serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kumfungia msanii Snura Mushi “Snura” kufanya maonyesho nchini pamoja na kuufungia wimbo wake wa Chura msanii huyo leo amejitokeza na kuomba msamaha.
Snura amesema kuwa anakiri kuwa nyimbo hiyo inaonyesha vitendo vya udhalilishaji na kwasasa amejisaliji BASATA na hivi karibuni wanataraji kufanya video nyingine ya wimbo wake wa Chura.
Amesema awali walikuwa hawajawa na elimu ya kutosha lakini kwa sasa anatambua nini anafanya na kuahidi kuwa balozi kwa wasanii wenzake.
“Tayari nimejisajili BASATA na sasa naruhusiwa kufanya onyesho hata leo usiku, tumefanya taratibu zote na tayari najulikana BASATA nimejisajili jana na cheti nimepewa,
DSC_1092
Snura akielezea kuhusu nyimbo yake ya Chura na makosa yaliyokuwepo kwenye video. Kulia ni meneja wake HK.
“Mwanzoni nilijua kujisajili COSOTA inatosha maana nilijisajili tangu 2009 lakini kumbe na BASATA natakiwa kujisajili … mimi sijafungiwa aliyefungiwa ni chura na tukifanya marekebisho itarudi kuwa kama kawaida,” amesema Snura.
DSC_1109
Snura na meneja wake HK wakionyesha vyeti baada ya kukamilisha usajili BASATA.
Kwa upande wa Meneja wake, Hemed Kavu “HK”, amesema kwa upande wao waliona ni sahihi kutoa video kama hiyo lakini tayari wamefahamu makosa na kuahidia kutokurudia tena.
Amesema kuwa anawashauri wasanii wengine kufuata sheria na kujisajili BASATA ili waweze kutambulika kisheria kwa kutambulika na serikali.
“Wasanii wengi hawatambuliki BASATA nitumie nafasi hii kuwashauri wajiunge ili wafanye kazi kwa kutambulika,” amesema HK.
DSC_1082
Hemed Kavu “HK” akizungumzia video ya Chura na maandaliziya video nyingine. Kulia ni msanii Snura Mushi “Snura”.
Kuhusu video ya Chura amesema tayari wameifuta mtandaoni na wameshapeleka mwongozo wa video nyingine ya Chura kwa BASATA na wanasubiri majibu ili waanze kuishuti.