Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, May 5, 2016

MABONDIA WA NGUMI ZA KULIPWA WAAHIDI WATANZANIA RAHA



 
 
HOMA ya pambano la kimataifa umezidi kupamba moto baada ya kukutanishwa mabondia wote  watakaocheza na mabondia wa nje na kuongea na waandishi wa habari.

Akizungumza na wandishi wa habari mratibu wa pambano hilo Anthony Rutta amesema mabondia wote wapo fiti kwa ajili ya mpambano huo wa kimataifa

“Bondia Thomas Mashali 'Simba Asiyefugika' atakuwa anagombea ubingwa wa dunia kg 76 mkanda wa U.B.O na Sajjad Mehrab kutoka Iran na Cosmas Cheka atakuwa akigombania ubingwa wa Dunia  wa U.B.O uzito wa super Feather kg 59  dhidi ya mkenya Francis Kimani” , alisema Rutta
 
Mapambano mengine ya kimataifa yatawakutanisha mabondia  Mwanadada Lulu Kayage atakaezichapa na Chiedza Homakoma 'Nikita' wa Malawi  wengine ni Ramadhan Shauri atakaepambana na Osgood Kayuni wa Malawi wakati Twaha Kassim atapambana na Fred Nyakese kutoka Kenya.

Saleh Mkalekwa atakumbana na James Onyango wa Kenya na Francis Miyeyusho atavaana na Frank Kiwalabye wa Uganda na Nassibu Ramadhani atacheza na Edward Kakembo wa Uganda Abdalla Pazi 'Dulla Mbabe' atavaana na  Chamunorwa Gonorenda kutoka Zimbabwe.

Shaban Kaoneka atacheza na Hassan Mwakinyo na Issa Nampepeche atakumbana na Baina Mazola na siku hiyo kutakuwa na burudani mbalimbali.


No comments:

Post a Comment