Tamasha
la Filamu la Zanzibar (ZIFF) linataraji kuanza mwezi Julai, 9 hadi
Jula, 17 huku filamu 80 zikitarajiwa kushiriki katika tamasha hilo kubwa
la filamu visiwani Zanzibar.
Akizungumzia
tamasha hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa ZIFF, Martin Muhando amesema kuwa
kwa mwaka 2016 walipokea maombi ya filamu 490 ambazo ziliomba kushiriki
tamasha hilo lakini wamepitisha filamu 80 ambazo zitakuwa katika
vipengele vitano.
“Wachambuzi
wamechagua makundi matano, kutakuwa na kundi la filamu za kawaida
litakuwa na filamu 59, Sembene Ousmmane 15, Filamu za Tanzania 12 na
filamu tano zitakuwa zinahusu Zanzibar na mshindi atapata tuzo ya
Emerson,” amesema Muhando.
Mkurugenzi
Mtendaji wa ZIFF, Martin Muhando akizungumzia tamasha la mwaka huu.
Kulia ni Meneja wa Tamasha la ZIFF, Daniel Nyalusi na Lilian Lundo
kutoka Habari Maelezo.
Amesema
kwa mwaka huu maombi yaliongezeka ambapo filamu za Tanzania walipokea
40 na kati ya hizo tano zitashindana katika kipengele cha Ousmmane na
kiujumla Tanzania imeingiza filamu 8, Kenya 5, Uganda 3 na Kenya.
Aidha
aliongeza kuwa katika tamasha la mwaka huu kutakuwa mashindano ya video
za muziki na kutakuwa na filamu mpya tatu ambazo hazijaambulishwa
sehemu yoyote na katika ZIFF ndiyo itakuwa sehemu ya kwanza.
Meneja
wa Tamasha la ZIFF, Daniel Nyalusi akizunguzia mabadiliko ya tamasha
kwa mwaka 2016. Kulia ni Meneja Mtendaji wa ZIFF, Martin Muhando na
Zuhirah Khaldun kutoka Diarra.
No comments:
Post a Comment