TIMU ya
Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imetua salama
jijini Goa, India kwa ajili michuano maalumu ya soka ya kimataifa kwa vijana
(AIFF Youth Cup 2016 U-16) yaliyoandaliwa na Shirikisho la Soka nchini humo
(AIFF).
Akizungumza
na wandishi wa habari, Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Alfred
Lucas alisema Mkuu wa msafara wa timu hiyo, Ayoub Nyenzi amesema wamepokelewa
vizuri na wenyeji India na jana asubuhi wachezaji walipumzika lakini jioni
walifanya mazoezi mepesi.
“Napenda kuwajulisha kuwa timu imefika salama
katika Jiji la Goa na tumepokelewa vizuri na wenyeji wetu. Kwa muda huu wa asubuhi
wachezaji watapumzika, jioni wataanza
program ya mazoezi,” amesema Nyenzi.Michuano hiyo ilianza jana na inachezwa kwa mfumo wa ligi kwa timu tano kucheza mechi nne na itaika tamati Mei 25
AIFF kimeandaa mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kikosi chao kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia kwa Vijana zitakazofanyika nchini humo mwaka 2017.
Wakati huo huo Shirikisho la Soka Afrika (CAF), limewateua waamuzi wanne kuchezesha mchezo Na. 27 kati ya Ethiopia dhidi ya Ghana kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana 2017 utakaochezwa Uwanja wa Addis Ababa, jijini Addis Ababa huko Ethiopia.
Mchezo huo utachezwa Mei 22, 2016, saa 10.00 jioni kwa saa za Ethiopia, utachezeshwa na mwamuzi Mfaume Nassoro na atasaidiwa na Josephat Bulali na Alli Kinduli na mezani atakuwa Martin Sanya na Kamishina ni Julius Mukolwe kutoka Kenya.
No comments:
Post a Comment