Kufuatia
majadiliano na vikao mbalimbali vilivyofanyika mwaka 2005-2010,
kumbukumbu zinaonyesha kuwa suala la uanachama wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) na Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA)
lilifanyiwa kazi kwa ukamilifu na Serikali za pande zote mbili kwa
ushirikiano na Vyama vyote viwili.
Hayo
yamesemwa leo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.
Nape Nnauye (Mb) wakati akijibu swali la Mhe. Mbunge wa Dimani Hafidh
Ali Tahir lenye kipengele a,b na c lililotaka kujua ni nini matokeo ya
Kamati iliyoundwa na Waziri Mkuu.
Mhe.
Nnauye ameeleza kwamba, kwa kutambua umuhimu wa ZFA kupata uanchama wa
FIFA, mwaka 2010 ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwamba,
ukiongozwa na aliyekuwa Naibu Waziri Kiongozi, Mhe. Juma Shamhuna pamoja
na aliyekuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo,
Mhe. Joel Bendera walikwenda Zurich, Switzerland ambako walikutana na
Rais wa FIFA wa wakati huo.
Aidha,
Mhe, Nnauye amefafanua kuwa, katika msafara huo walifuatana na
viongpozi wa TFF na ZFA na madhumuni ya safari hiyo ilikuwa ni
kuwasilisha maombi ya ZFA kupewa uanachama wa FIFA.
“Mwezi
Juni 2011, FIFA iliiandikia ZFA ikiwajulisha kuwa kwa mujibu wa
taratibu zilizopo, isingewezekana Zanzibar kupata Uanachama wa FIFA kwa
kuwa wananchama wao ni nchi zinazotambuliwa na Jumuiya ya Kimataifa kama
ilivyoelezwa katika aya ya 10 ya Katiba yao”, alisema Mhe. Nnauye.
Mhe.
Nnauye aliongeza kuwa, suala la usajili wa TFF au ZFA linafahamika
vyema ndani ya Serikali ya Mapinduzi pamoja na Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
“Hata
hivyo, naomba kulihakikishia Bunge lako Tukufu kuwa, uanachama wa TFF
katika FIFA upo kwa mujibu wa muafaka wa pande zote mbili.
Kwa
kuzingatia utaratibu wa FIFA kuhusiana na suala hilo, Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo imewaelekeza TFF nao wako tayari kufanya
maridhiano na ZFA ili kukamilisha utaratibu wa wazi wa kukidhi mahitaji
ya Zanzibar kushiriki katika masuala ya FIFA kupitia TFF bila kuathiri
ushiriki wa klabu za Zanzibar katika mashindano yanayoandaliwa na
Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF).
No comments:
Post a Comment