Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, May 17, 2016

SERENGETI BOYS ANA KWA ANA NA INDIA

 
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 maarufu kama Serengeti Boys, Bakari Shime amesema hana wasiwasi kuwavaa India-wenyeji wa michuano maalumu ya soka ya kimataifa kwa vijana (AIFF Youth Cup 2016 U-16) yaliyoandaliwa na Shirikisho la Soka nchini humo (AIFF).

Shime ambaye kikosi chake kilitoka sare ya 1-1 na Marekani Jumapili ya Mei 15, 2016, kesho Jumanne kikosi chake kitawavaa India kwenye Uwanja wa Tilak Maidan, Vasco jijini Goa kabla ya kuahidi kuwatungua wenyeji hao kwenye michuano hiyo inayofanyika ikiwa ni kuipa baraka India kabla ya fainali za kombe la Dunia kwa vijana mwakani-2017.
Katika mchezo wa Jumapili Marekani ndio walioanza kutangulia kufunga bao dakika ya tano lililowekwa kimiani na Jean Julien wakati bao la kusawazisha la Serengeti lilifungwa na Mohammed Abdallah katika dakika ya 16.

Kwa mujibu wa ratiba, Serengeti Boys itacheza mchezo wake wa tatu dhidi ya Korea Kusini Mei 19, 2016 kabla ya kumalizia na Malaysia Mei 21, 2016. Fainali ya michuano hiyo itachezwa Mei 25 na kabla ya mchezo wa fainali, utachezwa mchezo wa mshindi wa tatu katika uwanja huo huo Tilak Maidan, Vasco, Goa nchini India.

Katika historia ya soka duniani, AIFF imeipa Tanzania heshima kuialika kwenye michuano hiyo ukiacha nyingine nyingine za Afrika zenye mafanikio makubwa ya soka kwa kuipa nafasi Serengeti Boys ambayo inalelewa na Shirikisho la Soka Tanzania chini ya uongozi wa Rais Jamal Malinzi.
Mashindano hayo ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, ni sehemu ya maandalizi ya kikosi chao kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia kwa Vijana zitakazofanyika nchini humo mwaka 2017.

Kikosi cha Serengeti:
Kikosi hicho cha wachezaji 22, kiko chini ya Kocha Bakari Shime na kinaundwa na makipa, Ramadhan Kabwili, Kelvin Kayego na Samwel Brazio wakati mabeki wa pembeni ni Kibwana Shomari, Nicson Kibabage, Israel Mwenda na Ally Msengi.

Mabeki wa kati ni Issa Makamba, Nickson Job na Ally Ng'anzi huku viungo wakiwa ni Maulid Lembe, Asad Juma, Kelvin Naftari, Yasin Mohamed na Syprian Mwetesigwa na washambuliaji ni Aman Maziku, Rashid Chambo, Enrick Nkosi, Yohana Mkomola, Mohamed Abdallah, Shaban Ada na Muhsin Mkame.

Maofisa watakaosafiri na timu hiyo ni pamoja na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa TFF, Ayoub Nyenzi, Mshauri wa ufundi wa timu za vijana, Kim Poulsen, Kocha Mkuu, Bakari Shime, Kocha wa Makipa Mohamed Muharami, Daktari wa timu, Shecky Mngazija na mtunza vifaa, Edward Edward.
You might also like:

No comments:

Post a Comment