Wengi inaweza kuwachanganya na kushindwa kuelewa nini maana ya kusema makazi Liverpool na moyo Sevilla lakini huo ndiyo ukweli kuhusu beki wa kushoto wa Liverpool, Alberto Moreno.
KKijana huyu ambaye anaonekana kuwa na shughuli kubwa awapo uwanjani alizaliwa Sevilla nchini Hispania na alicheea klabu ya Sevilla kwa miaka 10 na baadda ya hapo alisajiliwa na Liverpool Agosti, 2014 kwa kitita cha Pauni Milioni 12.
345434A000000578-0-image-a-1_1463568941461
Tattoo ya Moreno iliyojichora katika mguu wake wa kulia iliyo na maneno Plaza de Espana in Seville
Akiizungumzia Sevilla kabla ya mchezo wa fainali ya Europa League ambao Liverpool ilifungwa goli 3-1, Morreno aliweka wazi kuwa yeye ni shabiki wa Sevilla.
“Nilizaliwa Sevilla, nilitokea Sevilla na mimi ni shabiki wa Sevilla,” alisema Moreno na kuongeza “Nilikuwa Sevilla kwa miaka 10 tangu nikiwa mdogo lakini kwa sasa ni mchezaji wa Liverpool nina furaha kuwa hapa na nimekuwa zaidi”
3455757F00000578-3596639-image-a-25_1463570693093

Moreno akiwa amebeba kombe Europa League ambalo Sevilla walilishinda baada ya kuifunga Liverpool.