Katibu Mkuu wa zamani wa klabu ya Yanga Dkt. Jonas Tiboroha amepata
dili jipya kunako klabu ya Stand United ya mkoani Shyinyanga.
Tiboroha anakuwa Mkurugengenzi Mtendaji Mkuu (C.E.O) wa Stand United
kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na uongozi wa klabu hiyo
iliyoanzishwa mwaka 2012.
Taarifa kutoka ‘Chama la wana’ inasomeka kama ifuatavyo: “Confirmed
Tiboroha sasa ni C.E.O wa Stand United, ungana nami kumpongeza na
kumtakia kila la kheri katika kazi yake. Tutamtambulisha kwa waandishi
wa habari siku ya Ijumaa kwenye ukumbi wa mikutano wa wadhamini wetu
ACACIA”.
Tiboroha alijiuzulu nafasi ya Ukatibu Mkuu katika klabu ya Yanga
akitoa sababu ya kuzongwa na majukumu mengi kutoka kwa mwajiri wake
‘mama’ ambaye ni Serikali kupitia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
|
Thursday, May 5, 2016
TIBOROHA AULA STAND UNITED
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment