FAINALI ya EUROPA LIGI ya Mwaka 2016 imechezwa huko St. Jakob-Park Mjini Basel Nchini Uswisi wakati Liverpool ilipoyeyuka Kipindi cha Pili na kutandikwa Bao 3-1 na Sevilla ambao sasa wamekuwa Klabu ya kwanza tangu Bayern Munich itwae Mataji Matatu mfululizo ya Ulaya.
Kati ya Mwaka 1974 na 1977, Bayern Munich ilitwaa Kombe la Ulaya mara 3 mfululizo na Jana Sevilla imeingia Vitabu vya Historia kwa kutwaa EUROPA LIGI kwa Miaka Mitatu mfululizo tangu 2014.
Ushindi huu umeifanya Sevilla sasa kuingizwa kucheza Makundi ya UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu ujao nafasi ambayo walikuwa hawana kwani kwao kwenye La Liga walikosa nafasi hiyo kwa kumaliza Nafasi za chini.
Sevilla sasa kucheza Uefa tena msimu ujao!Liverpool walianza vizuri na kumpa matumaini Meneja wa Jurgen Klopp kutwaa Taji kubwa la Ulaya kwa mara ya kwanza baada ya mara 4 zilizopita kufungwa Fainali na Timu zake pale Daniel Sturridge alipoipa Bao katika Dakika ya 35 na kuongoza 1-0 hadi Haftaimu.
Lakini Kipindi cha Pili waliyeyuka kwenye Mechi na kupigwa Bao 3 za Dakika za 46, 64 na 70 kupitia Kevin Gameiro na mbili za Andujar Moreno.
Hii ni Fainali ya Pili chini ya Jurgen Klopp kwa Liverpool kufungwa Msimu huu baada ya Mwezi Februari kubwagwa kwa Penati na Manchester City kwenye Fainali ya Capital One Cup.3-1Sevilla wakishangilia bao la kusawazisha dakika ya 46 kipindi cha piliMeneja wa Sevilla Unai EmeryVIKOSI:Liverpool walioanza XI: Mignolet, Clyne, Lovren, Toure, Moreno, Milner, Can, Lallana, Firmino, Coutinho, Sturridge
Liverpool akiba: Ward, Benteke, Henderson, Lucas, Allen, Origi, Skrtel
Sevilla walioanza XI: Soria, Mariano, Rami, Carrico, Escudero, Krychowiak, Nzonzi, Coke, Banega, Vitolo, Gameiro
Sevilla akiba: Sergio Rico, Kolodzieczak, Iborra, Cristoforo, Pareja, Konoplyanka, Llorente Mmiliki wa Klabu ya Liverpool John W Henry na Linda Pizzuti Henry wakiwa macho kwenye Uwanja wa St Jakob-Park leo kwenye kipute cha Fainali ya Uefa Europa Ligi.
No comments:
Post a Comment