Bayern
Munich Leo wametwaa Taji lao la 25 la Bundesliga huku wakiwa na Mechi 1
mkononi baada ya kushinda Ugenini Bao 2-1 walipocheza na Ingolstadt.
Huu ni Ubingwa wa 4 mfululizo wa Bayern
na hii imeweka Historia mpya huku Germany kwa Bayern kuwa Timu ya kwanza
kutwaa Ubingwa mara 4 mfululizo. Bao za Leo za Bayern zilifungwa na Robert Lewandowski na kumfanya aongoze Ufungaji Bora akiwa na Bao 29.
Moja ya Bao za Lewandowski ilikuwa ni Penati na Ingolstadt nao walifunga Bao lao kwa Penati ya Moritz Hartmann.
No comments:
Post a Comment