TIMU ya Ruvu Shooting imeingia kambini
jana kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao 2016/17 utakaoanza mwezi
Agosti.
Akizungumza na gazeti hili msemaji wa
timu hiyo Masau Bwire, alisema timu itaweka kambi ya mazoezi katika eneo la 832
Ruvu JKT, Uwanja wa Mabatini chini ya Kocha Mkuu, Tom Olaba akisaidiwa na
Seleman Mtungwe.
“Wachezaji waliripoti kambini juzi baada ya mapumziko mafupi waliyopewa baada ya kumalizika kwa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na tutafanya usajili kujaza nafasi za kipa, namba 2, 4, 6, 8, 9 na 10”, alisema Masau.
Pia Masau alisema lengo la kufanya usajili na kuanza kambi ya mazoezi mapema, ni kukiimarisha kikosi chao ili kiwe cha ushindani zaidi, msimu ujao wa ligi waweze kutwaa ubingwa wa soka Tanzania Bara.
Masau alisema wanataka kuja sawa kwenye ligi kama Leicester City ya England ilivyofanya kwenye ligi yao.

“Tuna imani kuyafikia malengo yetu
kwani, tunayo dhamira ya dhati kabisa, ndio maana tunaanza kambi mapema. Ombi
letu ni HAKI ifanyike kwa kila eneo wakati wote wa ligi, tunaweza, tutakuwa
mabingwa kwa uwezo wa kucheza mpira” alimalizia Masau
No comments:
Post a Comment