Serikali
kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imetoa motisha
kwa wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu wanawake(Twiga Stars)
ikishinda katika mchezo wake dhidi ya Zimbabwe unatarajiwa kuchezwa siku
ya Ijumaa tarehe Machi, 4 katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.
Haya
yamebainishwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Annastazia James Wambula alipotembelea kambi ya Timu hiyo leo jijini Dar
es Salaam.
Akizungumza
na wachezaji wa Twiga Stars, Wambura amesema kuwa Serikali kwa
kushirikiana na wadau wa michezo wamekusanya shilingi milioni 15 ambazo
zitatumika kama motisha kwa wachezaji hao.
Naibu
Waziri huyo aliongeza kuwa iwapo timu hiyo itaibuka na ushindi katika
mechi yake dhidi ya Zimbabwe kila mchezaji atapata gawio la sh. Laki
tatu kama motisha na kuongeza kuwa itafanyika hivyo hivyo katika mchezo
wa marudiano utakaochezwa nchini Zimbabwe.
Aidha
alitumia fursa hiyo kuwaomba wadau wa michezo kuzidi kujitokeza na
kuisaidi timu hiyo ikiwa ni pamoja na kuhudhuria kwa wingi katika mechi
ya tarehe Mach, 4 dhidi ya Zimbabwe itakayochezwa katika uwanja wa
Taifa.
Aliongeza
kuwa msaada zaidi unahitajika ili kuiwezesha timu hiyo kukidhi mahitaji
yake muhimu, hivyo alitoa wito kwa wadau mbalimbali kutoa michango yao
kupitia Twiga Specila Fund, Akaunti na: 20110001677 iliyoko NMB tawi la
Bank House jijjini Dar es Salaam.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesiga ameipongeza Serikali
kwa jitihada zake za kuhakikisha Twiga Stars inapata huduma muhimu
ikiwemo motisha kwa wachezaji na benchi la ufundi.
Mwesiga
pia amewapongeza wadau wote waliojitolea kusaidi timu hiyo ambapo
amesema kujitokeza kwa wadau hao kunaongeza morali ya wachezaji.
Msaada
huo wa shilingi milioni 15 umetolewa na wadau watatu ambapo mmja
aliyechangia shilingi Milioni 3 aliomba jina lake lihifadhiwe, wengine
ni Kampuni ya ASAS shilingi milioni 2 na Mamlaka ya Udhibiti wa
Mawasiliano Tanzania (TCRA) sh. Milioni 10.
Wakati
huohuo Waziri wa wizara hiyo, Mhe. Nape Nnauye amesema ili kuzidi
kuwatia moyo wachezaji hao atawaongezea laki nne kwa kila mchezaji kama
wataibuka na ushindi.
Mhe.
Nnauye alisema hayo wakati akizungumza na kipindi cha E sport
kinachorushwa na E fm na hivyo kupitia zawadi hiyo ya laki saba kwa kila
mchezaji anaamini itaweza kuwapa motisha wachezaji ya kufanya vizuri
katika kila mchezaji.
Na Frank Shijja
Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Selestine Mwesiga
akitoa shukura kwa Serikali kutokana na jitihada zake za kuitafutia
wadhamini Timu ya Taifa ya Mpira wa miguu wanawake (Twiga Stars) wakati
Naibu Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James
Wambura(wapili kutoka kushoto) alipo watembelea wachezaji wa Timu hiyo
leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Mjumbe wa Baraza la Michezo la
Taifa BMT Bi. Jeniffer Mmasi Shang’a (kulia). Kaimu Mkurugenzi wa
Maendeleo ya Michezo Makoye Nkenyenge.
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James
Wambura akisalimiana na Kocha wa Timu ya Taifa ya mpira wa Miguu
wanawake “Twiga Stars” (Nasra Juma) alipowatembelea kambini kwao leo
jijini Dar es Salaam. Katikati ni mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa
(BMT) Bi. Jeniffer Mmasi Shang’a.
Baadhi
ya wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu wanawake “Twiga Stars”
wakimsikiliza Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.
Annastazia James Wambura (hayupo pichani) alipowatembelea kambini kwao
leo jijini Dar es Salaam.Twiga Stars inatarajiwa kucheza mechi na Timu
ya Taifa wanawake ya Zimbabwe mchezo utakaochezwa tarehe 4 katika
uwanjja wa Taifa. (Picha na Wizara ya Habari)
No comments:
Post a Comment