Katika upigaji Kura wa kuchagua Mchezaji Bora, Rooney alizoa Kura Asilimia 54 akifuatiwa na Anthony Martial na Cameron Borthwick-Jackson waliopata Kura Asilimia 36 na 10.
Rooney aliuanza Mwezi Januari kwa kufunga Bao la ushindi Man United walipocheza na Swansea City akiunganisha kwa kisigino pasi ya Anthony Martial.
Kisha akafunga Penati iliyowapa Man United ushindi wa 1-0 walipoitoa Sheffield United kwenye EMIRATES FA CUP na kufuata Bao zake 2 Man United walipotoka 3-3 na Newcastle huko Saint James Park.
Lakini Mashabiki wa Man United watalikumbuka sana Bao lake huko Anfield wakati Man United wanawafunga Mahasimu wao wakubwa Liverpool 1-0.
Rooney alifunga Mwezi Januari kwa Bao jingine wakati Man United inaipiga Derby County 3-1 kwenyy e EMIRATES FA CUP na kutinga Raundi ya 5.
No comments:
Post a Comment