Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe akiongea na waandishi wa habari leo |
KITUO cha Televisheni cha ITV kimepewa tenda ya kuonyesha moja kwa moja onyesho la tuzo za muziki Tanzania, Kili Music Award itakalofanyika Juni 8, mwaka huu kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo katika ukumbi wa
Roots, Masaki, Dar es Salaam, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe
amesema kwamba sababu za kuichagua ITV ni kuamini wanaweza kufanya kazi hiyo
kwa ufanisi kulingana na makubaliano yao.
Pamoja na kurushwa live kupitia ITV, Kavishe amesema kwamba
onyesho hilo litaonyeshwa live katika sehemu tatu tofauti nchini, ambazo
wameziteua ni Mwanza eneo la Mabatini, Temeke Uwanja wa Taifa na Kilimanjaro, CCM
Mkoa.
Kavishe alisema zoezi la kupigia kura wasanii kuelekea tuzo
hizo zinazokwenda na kaulimbiu ya Kikwetukwetu mwaka huu lilifungwa Mei 31,
mwaka huu.
Pia Kavishe alisema wasanii wa sasa wataimba nyimbo za
wasanii wa zamani na wasanii wa zamani wataimba nyimbo za wasanii wa sasa.
“Kutakuwa na kitu tofauti kwa upande wa burudani, ambacho
kitapendeza na kuvutia, kwa ujumla maandalizi yako vizuri na tunatarajia mambo
mazuri siku hiyo,”alisema Kavishe.
No comments:
Post a Comment