Pages

Tuesday, November 3, 2015

DOKTA EVA CARNEIRO AMFUNGULIA MASHITAKA JOSE MOURINHO

ALIEKUWA Daktari wa Timu ya Chelsea Mwanamama Eva Carneiro amefungua Mashitaka dhidi ya Meneja wa Timu hiyo Jose Mourinho akidai ndie aliesababisha yeye kufukuzwa kazi kimakosa.
Tayari Dokta Carneiro ameshaishitaki Klabu ya Chelsea kwa kumtimua kinyume cha Sheria na sasa ameamua kumburuza Mourinho Mahakamani.
Sakata la Dokta Eva Carneiro na Mourinho liliibuka kwenye Mechi ya Agosti 8 ya Ligi Kuu England waliyotoka 2-2 na Swansea City Uwanjani Stamford Bridge.
Katika Mechi hiyo,Dokta Carneiro na Tabibu wa Viungo Jon Fearn waliingia Uwanjani kumtibu Eden Hazard kwenye Dakika za Majeruhi wakati Chelsea ipo 2-2 na Swansea City huku wakiwa Mtu 10 baada ya mapema Kipa wao Thibaut Courtois kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Kitendo hicho kilimkera Mourinho kwani Mchezaji akihudumiwa na Madokta basi huwajibika kutoka nje ya Uwanja na husubiri amri ya Refa kuingia tena huku Gemu ikiendelea na hilo liliiacha Chelsea iwe Mtu 9 kwa Dakika kadhaa.
Mourinho alimponda Dokta huyo na kumsema hajui mchezo unakwendaje.Mara baada ya Mechi hiyo na Swansea, Dokta huyo aliondolewa kuihudumia Timu ya Kwanza ya Chelsea.
Kuburuzwa Mahakamani kwa Mourinho kutazidi kumuongezea presha kwani hivi sasa Meneja huyo ambae yupo katika hali ngumu kutokana na Timu yake Chelsea, ambao ndio Mabingwa Watetezi, kufanya vibaya kwenye Ligi Kuu England wakiwa wamepoteza Mechi 6 kati ya 11 walizocheza na wanaselelea Nafasi ya 15 wakiwa Pointi 14 nyuma ya Vinara Man City.

No comments:

Post a Comment