Pages

Tuesday, November 3, 2015

UWANJA WA KAITABA BUKOBA WAANZA KUWEKWA NYASI BANDIA


Na Faustine Ruta, Bukoba
Uwanja wa Kaitaba Bukoba Umeanza kuwekwa nyasi bandia rasmi leo hii jumatatu 2 Novemba, 2015 na kutokana na maelezo ya wawekaji wamesema utachukuwa muda wa siku 14 tu.
Wakaazi wa Mji wa Bukoba na Vitongoji vyake sasa kuanza kushuhudia kipute live bila Chenga katika Uwanja huo wa Kaitaba. Timu ya Kagera Sugar nayo inatarajiwa kurudi katika Uwanja huo ambao uutumia kama Uwanja huo ambapo mpaka sasa tangu msimu uliopita wamekuwa wakitumia Viwanja vingine kwa michezo yao 
ya Nyumbani na Ugenini pia. Uwanja huu umejengwa kwa
ufadhili wa FIFA chini ya mpango wa misaada wa Goal Projects.

Uwekwaji Nyasi ukiendelea katika Uwanja wa Kaitaba leo hii.

Taswira ya Nyasi zenyewe za Bandia zikiwa zimetandazwa katika Uwanja huo wa Kaitaba uliopo Bukoba Mjini ambao hutumiwa na Timu ya Hapa Bukoba Kagera Sugar ambayo kwa sasa inaendelea kutumia Viwanja vya Ugenini.
Katibu wa KRFA Salumu Umande Chama ambaye pia ni Kiongozi kamati ya Waamuzi Nchini akizungumzia swala zima la Uwanja huo wa Kaitaba na Waandishi wa habari leo jumatatu 02 Novemba, 2015. Chama ameeleza kutokana na kasi iliyopo na kama Mafundi hawatakwama Uwanja huo utamalizika ndani ya Wiki mbili tuu.
Taswira kamili
Uwanja huo umeanza kuwekwa nyasi rasmi leo na ndani ya siku 14 utamalizika na taratibu nyingine zitafuata na Timu ya Kagera itaanza kuutumia Uwanja huo. Uwanja huu sasa utakuwa umeongezeka katika Viwanja vilivyowekwa nyasi hapa Tanzania ikiwa ni pamoja na Uwanja wa Uwanja wa Uhuru uliopo Dar es Salaam, Uwanja wa Karume (Dar es Salaam) na Uwanja wa Gombani uliopo Pemba.








No comments:

Post a Comment