Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, October 2, 2015

U15 YAICHAPA KOMBAINI TANGA 4-0



TIMU ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 15 (U-15) imeifunga Kombaini ya Tanga ya U-15 mabao 4-0  katika mechi zake za kujipima nguvu uliochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Mchezo huo uliochezwa juzi, ushindi ulitokana na mabao mawili ya Issa Abdi yaliyofungwa dakika ya 21 na 23, Frank George dakika ya tisa na Ibrahim Abdallah Ali dakika ya 80.
Pamoja na ushindi huo, vijana wa U-15 ya Taifa walikutana na ushindani kutoka kwa wachezaji wenye vipaji wa U-15 ya Tanga.
Kivutio zaidi alikuwa ni kiungo Joseph Yakobo ambaye Tanga wanamuita ‘Sure Boy’ na mshambuliaji George Chande aliyeisumbua mno ngome ya timu ya taifa iliyoongozwa na nahodha, Maulid Lembe.
Wachezaji wote waliokwenda majaribio Orlando Pirates ya Afrika Kusini mwezi uliopita, Asad Ali Juma, Issa Abdi Makamba, Kevin Deogratius Kahego, Amani Amede Maziku na Athumani Maulid Rajab walicheza.  
Huo unakuwa mchezo wa tano kushinda, kati ya mechi saba tangu kuundwa kwa timu hiyo Aprili mwaka huu, ikifunga jumla ya mabao 15 na kufungwa mawili tu.
Timu hiyo iliifunga  Mbeya 4-1 na 3-0, ikaifunga Zanzibar  4-0 na 1-0 na kutoka sare na Morogoro ya 0-0 na 1-1 na ushindi huu waTanga.
Timu hii inaandaliwa kwa ajili ya mechi za kufuzu Fainali za vijana Afrika mwaka 2017 nchini Madagascar zitakazoanza Juni mwakani, imekuwa ikiweka kambi kila mwishoni mwa mwezi kwa ajili ya michezo ya kujipima nguvu chini ya kocha Sebastian Nkoma.

No comments:

Post a Comment