Pages

Wednesday, October 28, 2015

RIGOBERT SONG ATEULIWA KOCHA WA TIMU YA TAIFA CHAD

Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon Rigobert Song ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Chad.
Song, mwenye umri wa miaka 39, aliteuliwa Jumatatu kumrithi Mfaransa Emmanuel Tregoat, ambaye mkataba wake ulimalizika Septemba 30.
"Haitakuwa rahisi kufuzu kwa Kombe la Taifa Bingwa Afrika 2017 lakini tuko tayari kujikaza kisabuni,” difenda huyo wa zamani wa Liverpool na West Ham amesema.
Kibarua cha kwanza kwa Song kitakuwa mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018 dhidi ya Misri Novemba.
Les Sao watakuwa wenyeji wa Misri kwenye mechi ya kwanza mjini N'Djamena tarehe 14 mwezi huu. Kutakuwa na mechi ya marudiano baadaye Misri.
Tregoat alifahamishwa mapema Septemba, baada ya kuchapwa 5-1 na Misri kwamba mkataba wake hautaongezwa.
Modou Kouta alifanywa kocha wa muda kandaa timu hiyo kwa mechi ya kufuzu kwa CHAN dhidi ya Gabon, ambayo walishindwa 2-1 kwa jumla.
Chad sasa wameweka matumaini yao kwenye Song, licha yake kukosa uzoefu katika ukufunzi.
Wakati wa uchezaji wake, Song alichezea Indomitable Lions mechi zaidi ya 100, na aliibuka Mwafrika wa kwanza kucheza katika fainali nne za Kombe la Dunia.

No comments:

Post a Comment