Pages

Wednesday, October 28, 2015

WAYNE ROONEY KUFANYIWA MECHI YA KUENZIWA 2016

Mchezaji wa Manchester United Wayne Rooney ameruhusiwa kufanyiwa Mechi ya Kumuenzi na mapato yote ya Mechi hiyo kwenda kwenye Mifuko ya Hisani.
Mechi hii imepitishwa baada ya Mashabiki kuiomba Klabu kutambua mchango mkubwa uliotukuka wa Rooney kwa Klabu hiyo.
Sasa Mechi hii itachezwa Old Trafford hao Agosti 3, 2016 dhidi ya Wapinzani ambao watapangwa baadae.
Akiongelea uamuzi huu, Rooney alisema: “Usiku wa Mechi utakuwa spesho kwangu na Familia yangu na nategemea tunaweza pia tukaleta kitu kimoja au viwili vya kushtukiza!”
Nae Mtendaji Mkuu wa Man United, Ed Woodward amesema: "Kuanzia Mechi yake ya kwanza aliyopiga Hetitriki hadi sasa ana Goli 236, Wayne amekuwa ndio Mtu mkuu
Katika kipindi cha mafanikio makuu ya Klabu!”
Habari hizi zimekuja wakati Oktoba 24 Rooney alitimiza Umri wa Miaka 30 na katika kipindi ambacho ananyooshewa kidole kuhusu uchezaji wake akiwa amefunga Bao 2 tu za Ligi katika Mechi 9 Msimu huu. Rooney, ambae alihamia Man United Mwaka 2004 akitoka Everton, ndie Mfungaji Bora wa 3 katika Man United akiwa nyuma ya Sir Bobby Charlton, Bao 249, na Denis Law, Bao 237, akiwa 1 tu mbele ya Rooney.
Mafanikio mengine ya Rooney akiwa na Man United ni kutwaa Ubingwa wa England mara 5 na UEFA CHAMPIONS LIGI mara 1.
Pia amebakisha Mechi 7 tu kuwa Mchezaji wa 10 kwa Man United kufikisha Mechi 500.

No comments:

Post a Comment