Pages

Wednesday, October 28, 2015

CAPITAL ONE CUP: LEO NI MAN UNITED vs MIDDLESBROUGH, MAN CITY vs CRYSTAL PALACE, LIVERPOOL vs BOURNEMOUTH

LEO Manchester United wako kwao Old Trafford kucheza Mechi ya Raundi ya 4 ya Kombe la Ligi, Capital One Cup, dhidi ya Middlesbrough ambayo ipo Daraja la chini la Championship.
Baada ya kutoka Sare na CSKA Moscow, kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI na Manchester City, kwenye Ligi Kuu England, Man United Leo wanapambana na Boro kwa mara ya kwanza tangu Msimu wa Ligi Kuu England wa 2008/09 wakati Boro iliposhushwa Daraja.
Wakati Man United inatoka kwenye Sare, Boro wanatoka Mechi yao ya Ligi ambayo waliichapa Wolves 3-1 baada ya kuwa nyuma kwa Bao 1-0 na kushika Nafasi ya 4 katika Daraja la Championship.
Kwenye Mechi hii, Man United itawakosa Majeruhi Antonio Valencia, Luke Shaw and Paddy McNair, Ashley Young na James Wilson lakini ipo nafasi kubwa kwa Chipukizi kutoka Brazil, Andreas Pereira, akacheza hasa baada ya kuchezeshwa na kufunga Bao katika Mechi ya Raundi iliyopita ya Mashindano haya dhidi ya Ipswich Town.
Nae Meneja wa Boro, Aitor Karanka, amedokeza huenda akapumzisha Wachezaji wake kadhaa ili kutilia mkazo kwenye Ligi yao wakawania kupanda Daraja kurudi Ligi Kuu England.
Lakini, huenda Boro wakamtumia mkongwe Stewart Downing, ambae aliwahi kuichezea England, hasa baada ya Jumamosi kufunga Bao safi la Friki walipoichapa Wolves.
Refa wa Mechi hii atakuwa Lee Mason.

Capital One Cup
Raundi ya 4
Saa 10:45 Usiku
Jumanne Oktoba 27

Liverpool v Bournemouth
Manchester City v Crystal Palace
Southampton v Aston Villa
23:00 Manchester United v Middlesbrough
Kikosi cha Man United kinaweza kuwa hivi:

No comments:

Post a Comment