Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, October 17, 2015

JOSE MOURINHO ASEMA HATAFUKUZWA HATA TUKIMALIZA NJE YA "TOP 4"

Jose Mourinho hana wasiwasi na kibarua chake kama Meneja hata kama Chelsea watamaliza Msimu huu wakiwa katikati ya Msimamo wa Ligi Kuu England.
Hivi sasa Chelsea, ambao ndio Mabingwa Watetezi, wapo Nafasi ya 16 kwenye Ligi baada ya Mechi 8 ambazo wamefungwa Mechi 4 na huu ni mwanzo wao mbovu tangu Msimu wa 1978/79.
Lakini Mourinho, ambae huu ni Mwaka wake wa pili tangu arejee tena kama Meneja na ambae mwanzoni mwa Msimu alisaini Mkataba mpya wa Miaka Minne, amesisitiza hana hatari ya kufukuzwa.
Alipohojiwa kama ana hakika atabaki kama Meneja hata kama Chelsea itamaliza Ligi ikiwa Nafasi za kati, Mourinho alijibu: “Ndio. Sikuambiwa hivyo kwa sababu sitegemei tutamaliza nafasi za kati kwenye Msimamo.”
Mara baada ya kuchapwa 3-1 na Southampton mapema Mwezi huu Uwanjani Stamford Bridge, Mourinho alisisitiza hataondoka Chelsea labda afukuzwe na Siku 2 baadae Klabu ya Chelsea ikatoa tamko kumuunga mkono.
Hatua hiyo ilimfurahisha mno Mourinho na kusisitiza hilo ni jambo muhimu mno kwake.
Hii Leo Chelsea wako kwao Stamford Bridge kucheza Mechi ya Ligi Kuu England na Aston Villa ambao wako Nafasi ya 18 zikiwa ni Nafasi 2 nyuma ya Chelsea wakiwa Pointi 4 nyuma yao.

No comments:

Post a Comment