Jumatano Raundi ya Mtoano ya Timu 16 pia itaendelea kwa Mechi mbili ambapo Mabingwa Watetezi Real Madrid watakuwa Wageni wa Schalke huko Ujerumani.
Msimu uliopita, Chelsea iliitoa PSG kwenye Robo Fainali za UEFA CHAMPIONS LIGI kwa faida ya Bao la Ugenini baada ya kupigwa 3-1 huko Parc des Princes katika Mechi ya Kwanza.

Msimu huu, kwenye hatua ya Makundi, Schalke pia walidundwa Bao 5-0 na Chelsea hapo hapo kwao na kupenya toka hatua hiyo baada ya kuifunga Sporting Lisbon 4-3 wakati Mabingwa Watetezi Real walivuka hatua ya Makundi kwa kushinda Mechi zao zote 6.
Mechi ya Pili ya Jumatano hiyo hiyo, ambayo itakamilisha Mechi za Kwanza za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ni kati ya Bayer Leverkusen na Atletico Madrid ambao ndio Washindi wa Pili wa UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu uliopita.
RATIBA:
Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku leo
Jumanne 17 Februari 2015
FC Shakhtar Donetsk vs Bayern Munich
Paris Saint-Germain vs Chelsea FC
Jumatano 18 Februari 2015
Schalke 04 vs Real Madrid CF
FC Basel 1893 vs FC Porto
No comments:
Post a Comment