Pages

Wednesday, October 21, 2015

FIFA BALLON D'OR: WAGOMBEA 23 WAANIKWA, RONALDO, MESSI WASHINDANI WAKUU

FIFA Leo imetangaza Listi ya Wachezaji 23 ambao watawania Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani wa Mwaka 2015, FIFA Ballon d'Or.
Miongoni mwa hao ni Cristiano Ronaldo, ambae ndie alietwaa Tuzo hiyo kwa Miaka Miwili iliyopita huku Lionel Messi akitajwa pia na ambae wengi wanadhani Mwaka huu ni zamu yake.
Mshindi Ballon d'Or huamuliwa kwa Kura inayohusisha Makocha na Makepteni wa Timu za Taifa Wanachama wa FIFA na Wawakilishi maalum kutoka Wanahabari.
Wagombea wote 23 wa Listi hii wanacheza Soka lao Barani Ulaya huku 11 wakitoka La Liga, 5 Ligi Kuu England, 5 toka Bundesliga na mmoja mmoja kutoka Ligi 1 na Serie A.
Klabu inayoongoza kwa kuwa na Wagombea wengi ni Bayern Munich yenye Wachezaji Watano ikifuatiwa na Real Madrid yenye Wanne. 

Kiinchi, Argentina na Germany, ambazo ndizo zilikutana Fainali za Kombe la Dunia za 2014 na Germany kuwa Mabingwa, ndizo zenye Wachezaji wengi wakiwemo Messi, Javier Mascherano, Sergio Aguero, Toni Kroos, Thomas Muller na Kipa Manuel Neuer.
Sherehe ya kutunuku FIFA Ballon d'Or itafanyika Tarehe 11 Januari 11 2016 huko Zurich, Uswsisi.

LISTI YA WACHEZAJI 23:
Sergio Aguero (Manchester City/Argentina)
Gareth Bale (Real Madrid/Wales)
Karim Benzema (Real Madrid/France)
Kevin De Bruyne (Manchester City/Belgium)
Eden Hazard (Chelsea/Belgium)
Zlatan Ibrahimovic (Paris Saint-Germain/Sweden)
Andres Iniesta (Barcelona/Spain)
Toni Kroos (Real Madrid/Germany)
Robert Lewandowski (Bayern Munich/Poland)
Javier Mascherano (Barcelona/Argentina)
Lionel Messi (Barcelona/Argentina)
Thomas Muller (Bayern Munich/Germany)
Manuel Neuer (Bayern Munich/Germany)
Neymar (Barcelona/Brazil)
Paul Pogba (Juventus/France)
Ivan Rakitic (Barcelona/Croatia)
Arjen Robben (Bayern Munich/Netherlands)
James Rodriguez (Real Madrid/Colombia)
Cristiano Ronaldo (Real Madrid/Portugal)
Alexis Sanchez (Arsenal/Chile)
Luis Suarez (Barcelona/Uruguay)
Yaya Toure (Manchester City/Ivory Coast)
Arturo Vidal (Bayern Munich/Chile)


LISTI YA MAKOCHA
Massimiliano Allegri (Italy/Juventus)
Carlo Ancelotti (Italy/Real Madrid)
Laurent Blanc (France/Paris Saint-Germain)
Unai Emery (Spain/Sevilla FC)
Pep Guardiola (Spain/FC Bayern Munich)
Luis Enrique Martinez (Spain/FC Barcelona)
Jose Mourinho (Portugal/Chelsea)
Jorge Sampaoli (Argentina/Chilean national team)
Diego Simeone (Argentina/Atletico Madrid)
Arsene Wenger (France/Arsenal)

No comments:

Post a Comment