Pages

Wednesday, October 21, 2015

YAYA TOURE KUSHINDANIA TUZO KUU YA SOKA DUNIANI

Wachezaji watatu wa Manchester City Sergio Aguero, Kevin De Bruyne na Yaya Toure ni miongoni wa wachezaji 23 walioorodheshwa kushindania tuzo ya Ballon d'Or.
Kiungo wa Chelsea Eden Hazard na mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez pia wamo kwenye orodha hiyo ya kuteua mchezaji bora wa mwaka duniani.

www.bukobasports.comTuzo hiyo ya Ballon d'Or kwa sasa inashikiliwa na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid ambaye pamoja na Lionel Messi wa Barcelona, wamekuwa wakishinda tuzo hiyo kwa miaka saba iliyopita. Wawili hao bado wamo kinyang’anyironi mwaka huu.
Mshambuliaji wa Real Madrid kutoka Wales Gareth Bale ndiye mchezaji Mwingereza pekee aliyetajwa kwenye orodha hiyo.
Meneja wa Chelsea Jose Mourinho na mwenzake wa Arsenal Arsene Wenger nao wamo kwenye orodha ya wakufunzi 10 watakaopigania tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka.
Watamenyana na meneja wa Barcelona Luis Enrique na kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola.
Katika orodha hiyo, La Liga ya Uhispania inaongoza kwa kuwa na wachezaji 11, nayo Bundesliga ya Ujerumani ina wachezaji sita. Serie A ya Italia ina wachezaji wawili.

http://www.bukobasports.comUfaransa inawakilishwa na mchezaji mmoja pekee, kigogo wa Paris St-Germain Zlatan Ibrahimovic.
  1. Sergio Aguero (Argentina/Manchester City)
  2. Gareth Bale (Wales/Real Madrid)
  3. Karim Benzema (France/Real Madrid)
  4. Cristiano Ronaldo (Portugal/Real Madrid)
  5. Kevin De Bruyne (Belgium/VfL Wolfsburg/Manchester City)
  6. Eden Hazard (Belgium/Chelsea)
  7. Zlatan Ibrahimovic (Sweden/Paris Saint-Germain)
  8. Andres Iniesta (Spain/FC Barcelona)
  9. Toni Kroos (Germany/Real Madrid)
  10. Robert Lewandowski (Poland/FC Bayern Munich)
  11. Javier Mascherano (Argentina/FC Barcelona)
  12. Lionel Messi (Argentina/FC Barcelona)
  13. Thomas Muller (Germany/FC Bayern Munich)
  14. Manuel Neuer (Germany/FC Bayern Munich)
  15. Neymar (Brazil/FC Barcelona)
  16. Paul Pogba (France/Juventus)
  17. Ivan Rakitic (Croatia/FC Barcelona)
  18. Arjen Robben (Netherlands/FC Bayern Munich)
  19. James Rodriguez (Colombia/Real Madrid)
  20. Alexis Sanchez (Chile/Arsenal)
  21. Luis Suarez (Uruguay/FC Barcelona)
  22. Yaya Toure (Côte d'Ivoire/Manchester City)
  23. Arturo Vidal (Chile/Juventus/FC Bayern Munich)

No comments:

Post a Comment