STRAIKA
Chipukizi wa Manchester United Anthony Martial ameteuliwa kuwa ndio
Mchezaji Bora wa Mwezi Agosti/Septemba katika Ligi Kuu England na kuzoa
Tuzo ya PFA ya Mashabiki.
PFA [Professional Footballers Association] ni Chama cha Kutetea Hakika Wachezaji wa Kulipwa wa Soka huko Uingereza.
Martial, mwenye Miaka 19, alijiunga na Man United katika Siku ya mwisho ya Dirisha la Uhamisho, hapo Septemba 1, kutoka AS Monaco ya France kwa Dau la Pauni Milioni 36.
Katika Mechi zake mbili za kwanza alifunga Bao 3 na kuwa Mchezaji Bora wa Mechi Man United walipoifunga Sunderland 3-0.
Ubora wa Martial ndio uliifanya Man United kutwaa uongozi wa Ligi Kuu England mwishoni mwa Septemba kitu ambacho walikuwa hawajafanya kwa Miaka Miwili.
Katika kinyang’anyiro cha Tuzo hii, Martial aliwabwaga Riyad Mahrez wa Leicester City na Mchezaji mpya wa West Ham Dimitri Payet.
Wachezaji wengine waliokuwemo kwenye Listi ya awali ya mchujo ni Bafetimbi Gomis (Swansea City), Odion Ighalo (Watford), Vincent Kompany (Manchester City), Graziano Pelle (Southampton), David Silva (Manchester City), Jamie Vardy (Leicester City), Callum Wilson (Bournemouth) na Ashley Williams (Swansea).Washindi wa Tuzo hii ya Mchezaji Bora wa PFA kwa Mashabiki hupatikana kila Mwezi kupitia Kura inayoendeshwa na www.skysports.com baada ya Wataalam kupendekeza Majina ya Wachezaji wanaogombea.
Jopo la Wataalam hao ni pamoja na Wachambuzi wa Soka wa Sky Sports Paul Merson, Ian Holloway na Peter Beagrie walijumuika na Mike Riley, Meneja Mkuu wa of the Professional Game Match Officials, [PGMO ni Kampuni inayosimamia Marefa wa Ligi] na Malcolm Clarke, Mwenyekiti wa Shirikisho la Mashabiki wa Soka, pamoja na Shabiki anaeshinda Tuzo ya kila Mwezi.

No comments:
Post a Comment