Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, October 2, 2015

ALIYEKUWA KOCHA KWENYE LIGI KUU YA UINGEREZA AJA TANZANIA KUONGOZA KITUO CHA VIJANA CHA MICHEZO

www.bukobasports.com

Ndugu Ray Power, ambaye amewahi kuwa Kocha wa Chama Cha Soka na mkuu wa kitengo cha mpira wa miguu katika chuo kiitwacho Central College Nottingham; ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi katika Kituo cha Vijana cha Michezo kilichopo Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam (pichani).

Katika nafasi yake mpya, Ndugu Power atasimamia mafunzo na Uongozi wa kituo kipya ambacho kinategemewa kufunguliwa tarehe 19 ya Mwezi huu. Ndugu Power anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkurugenzi wa kituo; Stewart Hall aliyejiunga na timu ya Azam kwa mara nyingine kama Kocha Mkuu

No comments:

Post a Comment