Pages

Saturday, September 5, 2015

TAIFA STARS YAIBANA NIGERIA TAIFA BAADA YA KUTOKA SARE YA BILA KUFUNGANA








TIMU ya taifa, Taifa Stars, leo ililazimisha sare ya bila kufungana na Nigeria ‘Super Eagle’ katika mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika, Afcon kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Mchezo huoa mabao ulikuwa wa kundi lao la G, Stars ilianza kwa kasi kwa timu zote kushambuliana, huku Nigeria ilianza kulifikia lango la Stars dakika ya kwanza, lakini beki, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ akaokoa shambulizi hilo.

Stars walijibu mashabulizi katika dakika ya tatu, wakati Mrisho Ngassa alipokimbia na mpira kuelekea kufunga, lakini shuti lake lilipanguliwa na golikipa wa Nigeria na kusababisha kona mabayo haikuwa na matunda yoyote.

Dakika ya tisa, Emmanuel Emenike alipiga kichwa kizuri kuelekea lango la Stars, lakini mpira ulitoka sentimita chache ya mwamba wa goli, huku Stars ikikosa goli dakika ya 12, baada ya Mbwana Samatta kuwapiga chenga mabeki, lakini shuti lake lilitoka nje.
Samatta tena katika dakika ya 21 alikaribia kuifingua bao Stars, lakini shuti lake la adhabu ndogo lilipanguliwa na golikipa wa Nigeria kwa ustadi mkubwa na kusababisha kona.

Ngassa na Samatta kwa nyakati tofauti walikosa nafasi nyingi na wazi za kufunga na hivyo kuufanya mchezo huo hadi kipenjya cha mwisho kinapulizwa, kuwa na matokeo tasa ya bila kufungana.
Kwa matokeo hayo, Stars sasa imefikisha pointi moja katika mechi mbili, baada ya mchezo wa kwanza kufungwa dhidi ya Misri.

Mara ya mwisho Tanzania kukutana na Nigeria ilikuwa Septemba 11, mwaka 2002 katika mechi ya kirafiki na Super Eagles ilishinda 2-0.
Lakini kwenye mechi za mashindano ilikuwa Desemba 20, mwaka 1980, katika mechi za kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia na Taifa Stars ikafungwa 2-0 Uwanja wa Taifa.

Huo ulikuwa mchezo wa marudiano baada ya awali Tanzania kutoa sare ya 1-1 Uwanja wa Surulele mjini Lagos, Nigeria Desemba 6, 1980. 


Matokeo ya mechi nyingine za kufuza kwa michuano hiyo ni Seychelles ilitoka sare ya kufungana bao 1-1 na Ethiopia, Sudan Kusini ikaibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Equatorial Guinea.
Mechi nyingine, Burundi ikaifunga Niger mabao 2-0, wakati Rwanda ilichapwa bao 1-0 na Ghana, huku Uganda wakiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Comoros na Senegal wakaifunga Namibia mabao 2-0.

No comments:

Post a Comment