Pages

Tuesday, September 8, 2015

RATIBA LIGI KUU ENGLAND JUMAMOSI, OLD TRAFFORD KUWAKA MOTO! NI MAN UNITED vs LIVERPOOL. KIPA MATATA DE GEA NDANI

David de Gea anaweza kuichezea Manchester United dhidi ya LiverpoolJumamosi hii inayokuja baada ya Kocha wa Spain Vicente Del Bosque kutoboa Kipa huyo wa Spain yupo tayari kuivaa Macedonia Jumanne kwenye Mechi ya EURO 2016.
Tangu Msimu huu mpya uanze, De Gea hajaichezea Man United hata Mechi moja baada ya Meneja Louis van Gaal kukataa kumteua wakati akiwa kwenye harakati za kuhamia Real Madrid mpango ambao ulishindikana Sekunde za mwisho.
Licha ya kuvumishwa kuwa kukwama kwa Uhamisho huo kumemfanya De Gea ahamanike, Del Bosque amesistiza kuwa Kipa huyo yuko fiti na tayari kuichezea Spain Jumanne huko Skopje.
Del Bosque ameeleza: “Yuko tayari kucheza. Yeye ni Mtu aliekomaa na hawezi kuathirika na kilichotokea. Nimeongea nae. Nilimuuliza kama yuko fiti kucheza na akajibu ndio. Tuna Kikosi kikubwa na ni wajibu kubadili Wachezaji.”
Kwenye Mechi yao ya Jumamosi ambayo Spain waliifunga Slovakia 2-0 na kutwaauongozi wa Kundi lao la EURO 2016, Del Bosque alimteua Kipa wa Iker Casillas kudaka.
Del Bosque alishamuonya De Gea kuwa kuteuliwa kuichezea Spain sasa kutalingana kama anapata namba Man United na kama hachezei Klabu yake basi hata Spain anaweza asiitwe.

No comments:

Post a Comment