Pages

Friday, September 4, 2015

KOCHA DEL BOSQUE AMTUPIA NENO DE GEA

KOCHA wa Timu ya Taifa ya Spain amesema Kipa David De Gea atajiamini zaidi kufuatia sakata lake la Uhamisho lililosababisha mvutano kati ya Klabu yake Manchester United na Real Madrid.
Vicente Del Bosque anaamini David de Gea anapaswa kufurahia mvutano huo kati ya Klabu kubwa kabisa Barani Ulaya.
De Gea alikuwa kwenye sakata la kuhamia Real Madrid lakini Uhamisho huo ulikwama Sekunde za mwisho hapo Agosti 31 baada ya Real Madrid kuchelewa kumsajili kwa wakati kwenye Mtandao wa FIFA wa Uhamisho wa Kimataifa, TMS [Transfer Matching System] na pia LFP, La Liga na kuziacha Klabu hizo mbili zikilaumiana.
Del Bosque amesema: “Lazima afurahie kwani Klabu kubwa zilikuwa zikimgombea. Sijaongea nae peke yake. Lakini anapaswa kufanya mazoezi. Yupo sehemu salama.” Mapema Del Bosque alimuonya De Gea kuwa lazima arejee kuwa Kipa Namba Moja wa Man United ndipo arejeshwe Kikosini Spain baada ya nafasi yake kuchukuliwa na Kipa wa Argentina Sergio Romero ambae amecheza Mechi zote 6 za Man United Msimu huu.

Hivi sasa De Gea yuko kwenye Timu ya Taifa ya Spain ikijitayarisha kucheza Mechi za Kundi lao la EURO 2016 Wikiendi hii dhidi ya Macedonia na Slovakia.
Akieleza zaidi, Del Bosque alisema: “"Jose Manuel Ochotorena [Kocha wa Makipa wa Spain] ameniambia De Gea yuko hali njema. Yupo amezungukwa na Juan Mata ambae ni Mtu mwema na hii itasaidia sana”

No comments:

Post a Comment