Pages

Thursday, September 3, 2015

NIKICA JELAVIC, ALEX SONG, ANTONIO, VICTOR MOSES WOTE NDANI YA WEST HAM UNITED

West Ham wamemsaini Kiungo wa Barcelona Alex Song na pia Winga wa Chelsea anaetoka Nigeria Victor Moses kwa Mkopo wa Msimu mmoja huku Straika wa Hull City Nikica Jelavic akitua kwa Dau la Pauni Milioni 3.
Song, Mchezaji wa Cameroun mwenye Miaka 27, aliichezea West Ham Mechi 31 Msimu uliopita akiwa hapo kwa Mkopo kutoka Barcelona ambako aliuzwa na Arsenal Mwaka 2012.

Moses, mwenye Miaka 24, hii Leo alisaini Mkataba mpya wa Miaka Minne na Klabu yake Chelsea lakini amepelekwa kwa Mkopo West Ham na hii ni Klabu yake ya Tatu kuichezea kwa Mkopo tangu ajiunge na Chelsea Mwaka 2012 na kupelekwa kuzichezea Liverpool na Stoke City.Nae Jelavic, Raia wa Croatia mwenye Miaka 30, anatarajiwa kusaini Mkataba wa Miaka Miwili na West Ham ambayo Meneja wao mpya ni Slaven Bilic aliekuwa Kocha wa Timu ya Taifa ya Croatia.
Antonio
LIGI KUU ENGLAND - UHAMISHO
  Uhamisho Uliofanyika mpaka leo.
-Anthony Martial [Monaco - Manchester United] £36m
-Virgil van Dijk [Celtic - Southampton] £11.5m
-Ramiro Funes Mori [River Plate - Everton] £9.5m
-Michail Antonio [Nottingham Forest - West Ham] Reportedly £7m
-Glenn Murray [Crystal Palace - Bournemouth] £4m
-Papy Djilobodji [Nantes - Chelsea] £4m

No comments:

Post a Comment