Pages

Thursday, September 3, 2015

MASHABIKI WA ARSENAL WATAKA KUJUA KWA NINI WENGER HAKUNUNUA WACHEZAJI WAPYA

The Arsenal Supporters’ Trust, Kundi rasmi la Mashabiki waliokubuhu wa Klabu ya Arsenal, wametangaza vita na kutaka ufanywe uchunguzi rasmi na wa haraka juu ya msimamo wa Klabu hiyo kuhusu Ununuzi wa Wachezaji baada ya Jana Meneja wao Arsene Wenger kutonunua Mchezaji hata mmoja wakati Dirisha la Uhamisho linafungwa.
Kuelekea Msimu huu mpya, Wenger alimnunua Mchezaji mmoja tu ambae ni Kipa Mkongwe kutoka Chelsea, Petr Cech, kwa Pauni Milioni 10 na kuruhusu Wojciech Szczesny, Lukas Podolski na Abou Diaby wote kuondoka.
Inaaminika Arsenal walikuwa wakihaha hiyo Jana Dakika za mwisho kusaini Wachezaji wapya na kushindwa na baadhi ya walengwa wao ni Mastraika Karim Benzema na Edinson Cavani.
Lakini inadaiwa Wenger hakuafiki ununuzi wao kwa Dau kubwa na kuridhika kuwa na Olivier Giroud, Danny Welbeck, Theo Walcott na Alexis Sanchez huku pia Mchezaji wao wa Costa Rica Joel Campbell akirudi Klabuni baada ya kumkatalia Mkopo huko France na Klabu ya Rennes.
Kundi hilo la Mashabiki pia limenyoosha kidole hali tete ya Kiungo chao ambapo wapo Francis Coquelin na Mikel Arteta wakati Jack Wilshere huwa majaribuni mara kwa mara kutokana na maumivu.
Kundi hilo limedai Wenger alikuwa na Bajeti ya zaidi ya Pauni Milioni 50 kununua wapya lakini wakachukizwa kwa nini Wenger hakuitumia hata xhembe kuimarisha Kikosi chao.

No comments:

Post a Comment