Pages

Tuesday, September 22, 2015

MURO NA TAMBO ZAKE DHIDI YA MECHI YAO NA SIMBA



 ... Jerry Muro, amefiwa na baba yake mzazi, mzee Cornel Muro usiku wa
KUELEKEA kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Yanga na Simba, Mkuu wa kitengo cha habari wa Yanga, Jerry Muro amerusha kijembe kwa mahasimu wao.
Mchezo baina ya vigogo hao wa soka nchini utachezwa siku ya Jumamosi katika uwanja wa Taifa ikiwa kila timu imeshashinda michezo mitatu na kushinda yote.
Muro amewafananisha mahasimu wao Simba, na kisigino ambacho daima huwa nyuma si mbele.
 “Sisi si kama ‘wamchangani-Simba’ ambao ‘ kutwa’ hawaishi kuongea bila kutekeleza ila niseme wazi tumeshinda michezo yetu yote na tunaongoza ligi, tunachokifanya sasa ni kuendelea kuwa juu kuhakikisha tunatimiza wajibu kwani nafahamu kamwe  kisigino hakiwezi kuwa mbele, siku zote kimekuwa nyuma. Haitawahi itokee hao ‘ wamchangani’ wakakaa mbele yetu”, alijigamba Muro
Pia alisema Yanga imejipanga vizuri hivyo anawataarifu wapenzi na wanachama  popote pale walipo kuwa timu inaendelea vizuri na kambi ya maandalizi kuelekea mchezo wa Jumamosi.
 “Hatutakuwa kuwa wazungumzaji sana, tunawaomba mashabiki wetu watupe muda wa kujitathimini na tuwe na wakati mzuri wa kukitayarisha kikosi chetu ili mwisho wa siku tuweze kupata matokeo mazuri zaidi, maneno siyo yatakayofanya kazi”, alisema Muro ambaye timu yake imeweka kambi Pemba.
Yanga imeshinda mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa kwanza kisha wakashinda 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa pili, wakaifunga JKT Ruvu mabao na kufikisha alama 9 sawa na timu za Simba, Mtibwa Sugar na Azam FC ambazo pia zimeshinda michezo yao mitatu ya mwanzo msimu huu.
Yanga wanaongoza ligi kutokana na wastani wao mzuri wa magoli 8. Wamefunga magoli 9, wameruhusu nyavu zao kutikiswa mara moja.
Simba pia wameanza ligi kwa ushindi mfululizo, wameshinda 1-0 dhidi ya Africans Sports, kisha wakashinda 2-0 dhidi ya JKT Mgambo na mechi hizo zote mbili za mwanzo walichezea ugenini, Mkwakwani ,Tanga.
Mechi yao ya kwanza katika uwanja wa Taifa msimu huu walishinda 3-1 dhidi ya Kagera  Sugar FC Jumapili iliyopita lakini hilo halimtishi, Jerry ambaye amesisitiza Yanga inahitaji utulivu na muda zaidi kabla ya kuendeleza ushindi wao wa Jumamosi hii.

No comments:

Post a Comment