Pages

Tuesday, September 22, 2015

DIEGO COSTA AISHTAKIWA NA FA KWA VURUGU

Diego Costa amefunguliwa Mashitaka na FA, Chama cha Soka England, ya kuleta vurugu kwenye Mechi iliyochezwa Stamford Bridge Juzi Jumamosi na Chelsea kuifunga Arsenal 2-0.
Costa, mwenye Miaka 26, alimsukuma kwa mkono usoni Beki wa Arsenal Laurent Koscielny na pia kumwangusha chini na baada ya hapo kuvaana na Beki mwingine wa Arsenal, Gabriel Paulista, ambae alitolewa nje kwa Kadi Nyekundu kwa kumpiga Teke Costa.
Mbali ya Costa, pia Gabriel amefunguliwa Shitaka la kufanya vurugu huku Klabu zote mbili zikipanda kizimbani kujibu Shitaka la kushindwa kuzuia Wachezaji wao kuleta vurugu.
Costa amepewa hadi Jumanne Tarehe 22 Septemba Saa 2 Usiku, Saa za Bongo, kujibu Shitaka hilo.

FA imetoa ufafanuzi kwa nini imemfungulia Mashitaka Costa kwa kusema tukio lake halikuonwa na Refa Mike Dean hivyo likapelekwa kwa Marefa Watatu wa zamani ambao waliupitia Mkanda wa tukio na wote waliafiki alipaswa kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Gabriel na Klabu hizo mbili, Chelsea na Arsenal, zimepewa hadi Alhamisi Septemba 24 kujibu Mashitaka yao.

No comments:

Post a Comment